July 30, 2016


Unaweza kutamka vyovyote, lakini Zlatan Ibrahimovich au Ibra Kadabra ni mtu hatari sana. Kwani ndani ya dakika 3 tu baada ya kuingia uwanjani ameifungia Man United bonge la bao kwa ile staiki ya “Kiki ya Baiskeli”.

Mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Ulevi jijini Stockholm, Sweden na huu ni uwanja ambao Zlatan ameuzoea kwelikweli.

Zlatan amefunga bao na kuisaidia Man United kushinda kwa mabao 5-2 katika mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Galatasaray ya Uturuki.

Mkali huyo raia wa Sweden mwenye asili ya Yugoslavia, amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na PSG kufikia kikomo.

VIKOSI
MAN UNITED:
 De Gea; Valencia, Bailly, Blind, Shaw; Schneiderlin, Herrera; Mkhitaryan, Rooney, Martial; Ibrahimovic.
Substitutes: Johnstone, Romero, Darmian, Jones, Rojo, Carrick, Fellaini, Lingard, Mata, Memphis, Young, Rashford.
GALATASARAY:
 Muslera; Linnes, Chedjou, Hakan, Carole, Selçuk, Dzemaili, Yasin, Sneijder, Bruma, Sinan.
Substitutes: Gonen, Aziz, Altintop, Donk, Bassan, Dursun, Unsal, Sarioglu, Iscan, Guney, Vatansever.






1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic