August 24, 2016

Kesi inayomhusu Mkurugenzi wa Kampuni ya Tiptop Connections, Hamis Taletale 'Babu Tale' ilipangwa kuendelea leo ambapo mshitakiwa huyo alitakiwa kufika mahakamani kujieleza ni kwa nini asifungwe jela baada ya kushindwa kulipa Sh milioni 250.

Tale ambaye ni meneja wa mwanamuziki, Diamond Platnumz, alifika katika Mahakama Kuu, leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kesi hiyo lakini imeahirishwa kwa mara nyingine baada ya Msajili wa Mahakama, Projestus Kahyoza aliyekuwa akishikilia kesi hiyo kuwa nje ya mkoa.


Tale anaandamwa na kesi ya kutakiwa kulipa fidia ya shilingi milioni 250 aliyofunguliwa na Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Shehe Hashimu Mbonde fedha baada ya kudaiwa kuuza kanda za mahubiri yake bila ridhaa yake.
Kesi hiyo ambayo Agosti 10, mwaka huu iliahirishwa kutokana na kukosekana kwa baadhi ya mawakili wa Tale, leo imeahirishwa tena kutokana na kukosekana kwa msajili huyo na sasa imepangwa kutolewa hukumu Septemba 12, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV