August 24, 2016

Kiungo wa Manchester United, Mjerumani Bastian Schweinsteiger, amesema baada ya kuondoka ndani ya kikosi hicho, hafikirii kujiunga na timu nyingine ya barani Ulaya, na badala yake ataenda kucheza soka katika Ligi ya Marekani au Asia.

Schweinsteiger ambaye amekuwa hafanyi mazoezi na kikosi cha kwanza cha United kutokana na kutokuwepo kwenye mipango ya kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, bado ameonyesha nia ya kuendelea kubaki klabuni hapo.


Kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter, Schweinsteiger aliandika: “Manchester United itakuwa klabu yangu ya mwisho hapa Ulaya. Naziheshimu klabu zingine, lakini Manchester United ndiyo timu pekee iliyonifanya nikaihama Bayern Munich. Nipo tayari kubaki kama timu hii itaendelea kunihitaji.
 


“Hiki ndicho ninachoweza kukisema kuhusiana na hatma yangu ya sasa. Napenda kuwashukuru mashabiki kutokana na ushirikiano waliouonyesha kwangu.”

Mjerumani huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha Ujerumani kilichotwa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014, mshahara wake ndani ya United ni pauni 160,000 kwa mwaka na mkataba wake umebakia miaka miwili kumalizika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV