August 31, 2016



Maelfu ya wadau wa soka, ndugu jamaa na marafiki wamejitokeza kuuaga mwili wa Munishi Boniventura ambaye ni baba wa kipa namba moja wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’.


Kati ya wengi waliojitokeza walionekana ni wadau wa soka na hasa mashabiki wengi wa Yanga wakifuatiwa na wale wa watani wao wa jadi Simba.

Watu hao walijitokeza kwa wingi kwenye Kanisa Katoliki Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam.


Baada ya shughuli hizo za kuaga, mwili ulipelekwa kwenye gari na msafara kwenda mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi ukaanza.

Wengine waliojitokeza ni baadhi ya viongozi wa Yanga, baadhi ya wachezaji na wale wa benchi la ufundi kuungana na kipa huyo ambaye baba yake mzazi aliugua kwa muda mrefu kabla ya mauti kumfika siku chache zilizopita.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic