August 17, 2016Straika nyota wa Simba, Laudit Mavugo, pamoja na wachezaji wa kigeni waliosajiliwa Simba msimu huu, wamepangiwa nyumba maeneo ya Sinza kwa ajili ya makazi yao kwa muda wote ambao watakuwa wakiitumikia timu hiyo.

Mavugo ametua Simba hivi karibuni ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia klabu yake hiyo ya sasa ambapo hadi sasa, ameshafanikiwa kufunga bao moja katika mechi ya Simba Day dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba kilisema, Mavugo amekabidhiwa nyumba ambayo alikuwa akiishi aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Hamisi Kiiza, ambaye amemwagwa katika usajili uliopita.

“Mavugo na wenzie wamepatiwa nyumba maeneo ya Sinza, wachezaji wote wa kigeni wanaishi katika nyumba ambayo alikuwa akiishi (Hamisi) Kiiza ambapo huduma zote muhimu za kibinadamu zipo ndani pamoja na fenicha zote,  hivyo wao wanaishi tu.


“Kiiza alipoondoka aliiacha nyumba ile ikiwa wazi bila kuifunga lakini tunashukuru Mungu vitu vyote tulivikuta salama, hivyo imekuwa rahisi na kuwapatia wachezaji hao wa kimataifa mahali pa kuishi,” alisema bosi huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV