September 1, 2016



Mshambuliaji mkongwe wa Ireland, Robbie Keane ameaga rasmi kuichezea timu yake ya taifa akiwa na miaka 36.

Keane ameaga wakati Ireland ikiibabua Oman kwa mabao 4-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Aviva mjini Dublin, Ireland.

Pamoja na kuwa anaaga, Keane ambaye alikipiga nchini England kabla ya kuhamia Marekani, alifunga moja ya mabao safi kabisa hiyo jana.

Ameitumikia timu hiyo kwa jumla ya dakika 11,148, akiwa amecheza mechi 146 na kufunga jumla ya mabao 68.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic