September 14, 2016

Kuelekea pambano la watani wa jadi, kiungo wa pembeni wa Yanga, Juma Mahadhi amesema mabeki wa pembeni wa Simba, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Besala Bokungu anawajua vizuri na amepanga kuwakimbiza watakapokutana.

Timu hizo zinatarajiwa kukutana Oktoba Mosi, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


 Akizungumza na Championi Jumatano, Mahadhi alisema kutokana na ubora wa kikosi cha Yanga kwa sasa, haoni kama kuna timu itawazuia huku akisisitiza kwamba amejipanga kufanya vizuri siku hiyo.

Mahadhi aliongeza kuwa, hatishwi na safu ya ulinzi ya Simba hasa mabeki wa pembeni, Zimbwe Jr na Bokungu kwani tayari amewaona jinsi wanavyocheza na amepania kuwakimbiza.

“Kiukweli kwa sasa ndani ya Tanzania, Yanga ndiyo timu bora kutokana na kikosi ilichonacho pamoja na mafanikio ya ushiriki wa michuano mikubwa na ni ajabu kukaa kuihofia timu kama Simba kwa sababu tayari tumeshacheza na timu kubwa na ngumu kuliko hiyo,” alisema Mahadhi.


SOURCE; CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV