October 27, 2016


Hawa wawili ni wapinzani wakubwa, Jose Mourinho na Pep Guardiola, lakini ni uwanjani. Nje ya uwanja ni watu wanaofahamiana maana walifanya kazi pamoja katika kikosi cha Barcelona, Mourinho akiwa kocha msaidizi na Guardiola akiwa mchezaji, tena nahodha.

Baadaye wakaonyeshana kazi mmoja akiwa Real Madrid na mwingine FC Barcelona. Sasa Mourinho yuko Man United na Guardiola yuko Man City, upinzani unaendelea.

Mourinho safari hii ilikuwa ni zamu yake ya ushindi, ameshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Guardiola, hakuna ubishi, soka raha sana, hasa ukiwa hauna hasira.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic