October 22, 2016Azam FC imeitwanga JKT Ruvu kwa bao 1-0 katika mechi ngumu ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na nahodha John Bocco katika dakika ya 57 baada ya Azam FC kufanya mashambulizi mfululizo katika kipindi cha kwanza.


Kipondi cha pili kilionekana kuwa kigumu sana JKT Ruvu hasa mwanzoni kwa kuwa Azam FC walikuwa wakisukuma mashambulizi mfululizo, lakini hawakuwa makini katika umaliziaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV