October 22, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90 sasa, hakuna kipya, timu zinaonyesha kucheza zaidi katikati ya uwanja, Yanga wakiwa wameridhika huku Kagera wakionekana kuwa wamekata tamaa

Dk 87, mpira wa kurusha wa Twite, Tambwe anagonga kichwa lakini Babu Ally anaokoa
Dk 83 hadi 85 Yanga wanaendelea kucheza taratibu kwa kujiamini, lakini kama Kagera watazubaa, basi Yanga wanaweza kuongeza bao tena
Dk 82, Danny Mrwanda ambaye amefunikwa na Yondani anageuka na kujaribu shuti lakini Dida anadaka vizuri

Dk 79 hadi 81, Yanga wanaonekana kugongeana taratibu kwa mbwembwe kabisa,wakiupoza mchezo
SUB Dk 78, Matheo Anthony anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke
SUB Dk 77, Amissi Tambwe anaingia upande wa Yanga kuchukua nafasi ya Obey Chirwa
GOOOOOOO Dk 73, Ngoma anaifungia Yanga bao la sita, ameunganisha pasi ya MSuva baada ya kumzidi kasi Kavila
Dk 72 Kagera wanapata kona na kushambulia, lakini inaonekana haina madhara na Yanga wanaokoa

 Dk 72 Kagera wanapata kona na kushambulia, lakini inaonekana haina madhara na Yanga wanaokoaGOOOOOO Dk 63, Chirwa anafunga bao la tano kwa Yanga, la pili kwake baada ya Ngoma kuuwahi mpira wa Juma Ramadhani aliyemrudishia kipa, lakini kipa Burhani akaokoa, mpira ukamkuta Chirwa ambaye amemlamba chenga na kupachika wavuni kwa mguu wa kushoto safi kabisa
SUB Dk 60, anaingia Babu Ally kuchukua nafasi ya Godfrey Taita upande wa Kagera
GOOOOOOO Dk 57, Kaseke anafunga bao kwa shuti kali kabisa akiunganisha pasi nzuri ya MSuva aliyegongeana vizuri na Niyonzima
DK 56, beki Juma ramadhani anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mzuri wa Niyonzima langoni mwake
Dk 55, krosi nzuri ya Niyonzima, Msuva akiwa katika nafasi nzuri lakini anashindwa kulenga. Beki wa kati wa Kagera wanaonekana kama kuzubaa hivi
SUB Dk 53, mkongwe Mbuyu Twite anaingia kuchukua nafasi ya Kessy ambaye ameumia
DK 52, Kessy wa Yanga yuko chini akipatiwa matibabu, anatolewa nje

Dk 52, Msuva anagongeana vizuri na Niyonzima ambaye anapiga shuti kali lakini hakulenga lango
Dk 50, Msuva anaingia vizuri lakini badala ya krosi anajaribu kupiga shuti na mpira unatoka juuuu, goal kick
GOOOOOOO Dk 48, Mbaraka Yusuf anaunganisha pasi fupi ya Mangoma na kuifungia Kagera Sugar bao la pili katika mchezo wa leo. Huyu ndiye aliyefunga bao la kwanza
DK Dk 46 Ngoma anaingia vizuri lakini anageuka na kumpa pasi Niyonzima, lakini mpira wake unakuwa laini
Dk 46, Mpira umeanza taratibu Kagera wakigonga pasi nyingi fupifupi

MAPUMZIKO 
-Hatari kabisa kwenye lango la Kagera, Ngoma anapiga free header lakini unatoka nje sentimeta chache kabisa

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, mpira wa krosi kali ya Taifa, Dida anapangua na mabeki wa Yanga wanaondosha
Dk 44 sasa, Yanga wanaonekana kuupoza mchezo na hawana haraka hata kidogo, wanagongeana taratibu kabisa hapa

Dk 40, Yanga wanagongeana vizuri, Mwinyi anapiga krosi tamu kabisa lakini Juma ramadhani anawahi kuokoa na kuwa kona. Inachongwa tena, haina manufaaa
Dk 38, Dida anafanya kazi ya ziada, anatoka nje ya 18 na kuokoa mpira miguuni mwa Ally 
Dk 37, Chirwa anaingia na kumdhibiti Juma Ramadhani, anatoa krosi safi kwa MSuva ambaye anapiga shuti, wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa na Niyonzima lakini haina matunda
Dk 35, Kagera wanafanya shambulizi, mpira mzuri na Mangoma anaachia shuti kali lakini Andrew Vicent anaweka kichwa na kuokoa
KADI Dk 33, Kessy analambwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Taita

DK 33, Ngoma na Msuva wanagongeana vizuri na krosi safi lakini Burhani anaokoa vizuri kabisa
SUB Dk 31 Kagera wanamuingiza Ali Ramadhani kuchukua nafasi Japhet Makaray, Pia wanamtoa kipa Casillas na nafasi yake inachukuliwa na David Burhani
Dk 30, Kagera wanaonekana kuwa wamepaniki sasa na wanakaba kibabe jambo ambalo linaweza kuwasumbua au kuwaponza kupata kadi
Dk 28 sasa, Yanga wanaonekana wanaendelea kushambulia kwa kasi zaidi wakiwapa Yanga 
GOOOOOOOOOO Dk 26, Niyonzima anatoa krosi safi kabisa, Msuva anaachia shuti, Casillas anaokoa tena lakini Chirwa anauwahi na kuutupia wavuni, Yanga tatu
KADI Dk 23, Selemani Mangoma wa Kagera analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ngoma kwa makusudi
GOOOOOO Dk 21, Niyonzima anageuka na kupiga shuti kali, Casillas anatema na Msuva anamalizia safi kabisa na kuiandikia Yanga bao la pili

Dk 15, Ufudu wa Kagera anafanya kosa hapa, anaingia Chirwa hatari lakini Juma Ramadhani anawahi na kuondosha hatari hiyo
DK 10 hadi 14, mpira zaidi unachezwa katikati ua uwanja na inaonekana timu zina nafasi ya kugongeana kwa kuwa uwanja ni safi kabisa
Dk 9 Japhet Makalay anaingia vizuri baada ya kumtoka Kessy lakini krosi yake inaishia mikononi mwa Dida
Dk 8, Msuva anaingia tena, krosi safi kabisa hatariiii lakini Casillas anatokea na hudaka vizuri kabisa
Dk 6, Mangoma wa Kagera anaingia vizuri anaachia shuti kali kabisa lakini ni goal kick
GOOOOOOOO Dk 5, Ngoma anaifungia Yanga bao la kusawazisha baada ya kufunga kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Simon Msuva
GOOOOOOOOOO Dk 3, Mbaraka Yusuf anamtoka Yondani na kuachia mkwaju mkali unaomngonga Dante na kumpoteza maboya kipa Dida na unajaa wavuni

Dk 1, Yanga wanaonekana kuanza kwa kasi kama wamepanga kupata bao la mapema ikiwezekana kumaliza kazi mchezo


Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Kagera Sugar

1. Deogratius Munishi
2. Hassani Kessy
3. Mwinyi Haji
4. Andrew Vicenti
5. Kelvin Yondani
6. Thabani Kamusoko
7. Saimoni Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Donald Ngoma
10. Obrey Chirwa
11. Deusi Kaseke

Akiba
- Beno Kakolanya
- Oscar Joshua
- Vicent Bossou
- Mbuyu Twite
- Geofrey Mwashuiya

- Mateo Antony

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV