October 22, 2016

MUZAMIRU (KATIKATI) AKIPAMBANA NA WALINZI WA MBAO FC YA MWANZA

Baada ya kuifungia Simba bao pekee na la ushindi dhidi ya Mbao FC juzi Alhamisi katika Ligi Kuu Bara, kiungo Mzamiru Yassin amesema huo ni mwanzo tu kwani amepanga kuendelea kufunga katika mechi zijazo.

Mzamiru licha ya kucheza mbali na goli kutokana na majukumu yake ya kiungo wa kati, hadi sasa amefunga mabao mawili katika ligi. Lingine alifunga dhidi ya Kagera Sugar ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.

Kiungo huyo alisema: “Kwa staili ninayocheza na majukumu yangu yalivyo, nitafunga zaidi katika mechi zinazokuja za timu yangu.

“Nacheza maeneo ambayo mpira unapatikana kwa wakati huo yaani ‘box to box midfield’, ndiyo maana nimeweza kufunga mabao ndani ya 18, sasa kwa staili hiyo nafikiri itakuwa ni kawaida yangu kufunga.

“Ukiangalia pia mimi binafsi napenda kuisaidia timu yangu kufunga mabao ili kupata ushindi, kwa hiyo ninapopata nafasi na ukizingatia majukumu yangu yalivyo uwanjani nitakuwa nafunga sana kila ninapopata nafasi,” alisema Mzamiru aliyetua Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar.   
Msimu huu Simba imesajili wachezaji watatu kutoka Mtibwa akiwemo Mzamiru, wengine ni Shiza Kichuya mwenye mabao saba katika ligi na Mohammed Ibrahim.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV