October 22, 2016


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ametoa miezi nane kukamilika kwa ujenzi wa uwanja wa mazoezi huko Gezaulole, Kigamboni jijini Dar es Salaam ambao utatumiwa na timu hiyo.

Manji, tayari amekabidhi eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 712 kwa Yanga, ambalo limetengwa kwa ajili wa ujenzi wa uwanja wa mazoezi na hosteli za timu hiyo.

Manji alisema ujenzi huo unatarajia kuanza kujengwa rasmi ndani ya siku 90 mara baada ya kufikia makubaliano kati yake na wanachama wa timu hiyo.

Manji alisema, kikubwa anataka kuona timu hiyo ikipata mafanikio kupitia kwa Kampuni ya Yanga Yetu ambayo itakodi timu na nembo ya Yanga.

“Tulitakiwa tuwe tushaanza ujenzi wa uwanja na hosteli kwenye eneo tulilopewa na Kampuni ya Yanga Yetu, lakini zoezi hilo tumelisitisha kutokana na malumbano yalikuwepo kati ya kampuni hiyo na wanachama.

“Hivyo, tumepanga kuanza ujenzi huo ndani ya siku 90 mara baada ya kufikia muafaka mzuri kati ya wanachama na Kampuni ya Yanga Yetu.


“Mimi kikubwa ninataka kuona Yanga ikipiga hatua za kimaendeleo katika soka, pia kama uongozi wangu niliahidi kuijengea Yanga uwanja mkubwa utakaotumika kwa ajili ya mechi kubwa za Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa tutakaoujenga Kaunda yalipo makao makuu yetu,” alisema Manji.

1 COMMENTS:

  1. Ni mpango mzuri na wenye maendeleo katika Club yetu pendwa, ila naomba itekelezwe kama ilivyo pangwa maana uliahidi wakati unaingia madarakani hapo yanga sc.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic