October 3, 2016Ukitaka mwanao apate shida, mwite Balotelli, maana hili jina, mwenyewe Mario Balotelli ni shida tupu.

Jana ameonyesha kweli ana uwezo wa kucheza soka, kafunga bonge la bao na kuisaidie Nice kushinda kwa mabao 2-1 katika Ligi ya Ufaransa.

Lakini baada ya bao hilo katika dakika ya 86 akavua jezi, akapigwa kadi ya njano. Baada ya hapo, dakika mbili baadaye akaanzisha mzozo na beki Steven Moreira, wakaanza kusukumana, akalambwa njano nyingine katika dakika ya 90, akatolewa nje.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV