October 27, 2016


Mtanzania bondia wa ngumi za kulipwa, Cosmas Cheka atapanda ulingoni dhidi ya Jason Bedemen raia wa Afrika Kusini ambaye awali alitakiwa kuzichapa na Mtanzania, Ibrahim Class kabla ya kuingia mitini nafasi yake kupewa Cheka.
Pambano hilo la raundi 12 litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar, litatanguliwa na pambano lingine la kimataifa kati ya Mtanzania.

Akizungumzia pambano hilo wakati wa kupima uzito, Cheka alisema kuwa: “Nimekuwa nikifanya mazoezi wakati wote kwa sababu kazi yangu ni bondia sina kazi nyengine zaidi ya hii manaa shule sikusoma, sasa lazima kesho huyo Mzungu atakiona cha moto na hivi alivyo mweupe mbona atafurahi na roho yake.”

Katika hali ya kushangaza, Bedemen aligoma kuongelea pambano hilo hali iliyomlazimu kocha wake, Manily Fernandes kusema kuwa: “Bondia wangu yupo vizuri kwa pambano ingawa bado anatatizika  na suala la kubadilishiwa mpinzani  tuliyeambiwa awali lakini kwakuwa tutalizungumzia hilo badaaye kabla ya kupanda ulingoni  ila kwa upande wa maandalizi  yupo vizuri na lazima amshinde mpinzani wake.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV