Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ kesho anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na Mchina, Chengbo Zheng katika pambano lisilokuwa la ubingwa ambapo amefunguka kuwa kichapo atakachompa hakitokuwa cha kawaida kwa upande wake kutokana na maandalizi aliyoyafanya.
Pambano hilo la raundi 12 litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar, litatanguliwa na pambano lingine la kimataifa kati ya Mtanzania, Cosmas Cheka dhidi ya Jason Bedemen raia wa Afrika Kusini ambaye awali alitakiwa kuzichapa na Mtanzania, Ibrahim Class kabla ya kuingia mitini nafasi yake kupewa Cheka.
Mbabe alisema kuwa anataka Watanzania wajitokeze kwa wingi katika pambano hilo kabla ya kumaliza kazi mapema kutokana na Mchina huyo kupotea maboya kwa kukubali kucheza naye kwani lazima akayanyage.
“Niwaombe Watanzania wenzagu wajitokeze kwa wingi kesho kushuhudia jinsi ninavyomfanya vibaya huyu jamaa kwa sababu anautambua moto wangu kutokana na kumchapa mwezake tena kwenye mji wao sasa huyu ameyakanyaga mwenye kwa kujileta hapa kwetu na hawezi kutoka bure.
Kwa upande wa Mchina huyo alisema kuwa: “Nimekuja Tanzania kwa kazi moja tu ya kuhakikisha namdondasha mpinzani wangu haijalishi yupo poje kwa sababu natetea taifa na nafsi yangu hivyo siwezi kuhofia chochote.”
0 COMMENTS:
Post a Comment