October 16, 2016

Yanga na Azam FC zimekutana leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuumana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara lakini kabla ya mchezo huo kuna tukuio lilifanyika uwanjani hapo.

Kabla ya mchezo huo, nahodha wa Azam FC, John Bocco alikabidhiwa tuzo yake ya kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti 2016 katika ligi hiyo.


Bocco  alipata tuzo hiyo baada ya kuwa na kiwango kizuri katika  ambapo aliwashinda Mzamiru Yasin wa Simba na Said Kipao wa JKT Ruvu waliokuwa wakiwania naye katika orodha ya wachezaji watatu waliongia hatua ya mwisho ya tuzo za mwezi huo.

Bocco aliifungia timu yake mabao matatu likiwemo la kusawazisha dhidi ya African Lyon.

Alifunga mabao mengine mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 wa timu yake dhidi ya Majimaji. Katika mechi hizo mbili, Azam FC ilifanikiwa kupata pointi nne kati ya sita.

Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili tu za Ligi hiyo iliyoanza Agosti 20, mwaka huu. Kwa kushinda tuzo hiyo, Bocco amezawadiwa kitita cha shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo, Kampuni ya Vodacom Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic