October 16, 2016



FULL TIME
Mchezo umemalizika, matokeo ni Azam FC 0, Yanga 0.
Dk 94, Mchezo unaweza kumalizika muda wowote kuanzia sasa.
Dk 93, Mchezo umekuwa na kasi ya kawaida, inaonekana pande zote zimeshaona utamalizika kwa suluhu.
Dk 92, dakika mbili za nyongeza zimekatika, mashabiki kadhaa wameanza kuondoka uwanjani.
Dk 90, mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 4 za nyongeza.
Dk 87, Azam wanafanya mabadiliko, anaingia Khamis Mcha, anatoka Kangwa.
Dk 85, Kangwa wa Azam anaumia mguu baada ya kuumizwa na Kelvin Yondani ndani ya eneo la 18 la Yanga wakati wakiwania mpira, lakini mwamuzi hakupuliza kipenga.
Dk 83, Azam wanafanya shambulizi kali, inapigwa kona Frank Domayo anapiga kichwa mpira unaelekea wavuni lakini Dida anafanya kazi nzuri, akauokoa mpira na mabeki wake wanaupiga kuuondoa langoni. Dk 80, Yanga wanafanya mabadiliko, Dante anatoka anaingia Nadir Haroub 'Cannavaro'. Dante aliumia baada ya kuchezewa faulo na kiungo wa Azam FC, Himid Mao.
Dk 78, Azam wanamtoa John Bocco, anaingia Francisco. 
Dk 76, Mwamuzi Israel Nkono anasimamisha mchezo kwa muda, anazungumza na Thomas wa Azam ambaye alionekana kupandwa na hasira na kumfokea mwamuzi wa akiba baada ya kuutoa mpira na kuelekea langoni kwake akidhani ulitakiwa kuelekea upande wa Yanga.

Dk 67, Kasi ya mchezo siyo kali, imepungua na mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja huku timu zote zikionekana kutegeana katika kufanya mashambulizi.
Dk 65, Msuva anaingia na mpira lakini anafanyiwa faulo na kiungo wa Azam, Migi.Dk 60,Yanga wanapata kona.Inapigwa kona lakini mabeki wa Azam wanaoko.

Dk 57, Yanga wanafanya mabadiliko, anaingia Geofrey Mwashiuya, anatoka Deus Kaseke ambaye alikuwa upande wa winga wa kushoto.
Dk 55, Kangwa wa Azam anapata nafasi ya kupiga shuti kali langoni mwa Yanga lakini Dida analidaka.
Dk 53, Azam wanafanya shambulizi lingine lakini kipa wa Yanga, Deo Munis 'Dida' anaokoa. 
Dk 50, Azam wanapiga pasi nzuri kuanzia katikati ya uwanja, wanalifikia lango la Yanga lakini mshambuliaji Thomas anashindwa kutumia nafasi anayopata, mabeki wa Yanga wanaokoa. 
Dk 47, Mchezo umeanza kwa kasi ndogo, bado timu zote zinaonekana kusomana.
Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO
-KADI Mudathiri kwa kuinua mguu juu ya kichwa cha Twite
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 44, Chirwa anaruka na kuunganisha krosi ya Msuva lakini inakuwa laini kabisa kwa Aishi
Dk 41, Bocco anaachia shuti kali kabisa, lakini Dida anaokoa na kuwa kona
Dk 36 hadi 40, hakuna shambulizi hata moja na mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja
Dk 34, Morris anafanya kazi ya ziada kukoa mpira mbele ya Chirwa na kuwa kona,inapigwa lakini haina faida
 Dk 32, Ya Thomas anaingia vizuri tena na Yanga wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na Mudathir, Yanga wanaokoa
Dk 29, krosi ya Ya Thomas inazuiwa na kuwa kona upande wa Yanga, Azam wanaichonga lakini haina makali, Yondania anaondosha 

SUB Dk 27, Mbuyu Twite anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul aliyeumia
KADI Dk 24, Morris analambwa kadi ya njano baada ya kwenda kumuangusha Chirwa
Dk 23, Mudathir anapiga shuti kali kabisa la mpira wa adhabu, Dida anaokoa vizuri na kuwa kona ya kwanza ya Azam FC
Dk 16, mpira wa adhabu wa Juma Abdul, kichwa safi cha Chirwa lakini Aishi anaonyesha anaweza na kudaka vizuri kabisa

Dk 15, Yanga inapata kona ya tano baada ya shuti la Kamusoko kuokolewa na mabeki wa Azam FC
Dk 13, Azam wanapoteza nafasi nzuri kabisa, krosi nzuri, Ya Thomas anaunganisha lakini kiduchu kabisa inatoka nje ya lango la Yanga
 Dk 10, Azam wanafanya shambulizi kubwa, lakini Yanga wanaokoa na Juma Abdul anachukua mpira na kuanza kazi
KADI Dk 7, Nyoni kalambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Msuva 
Dk 3, Yanga inapata kona ya tatu ndani ya dakika tatu, lakini inakuwa haina madhara tena kwa Azam
Dk 2, Msuva anaingia vizuri kabisa, lakini Azam FC wanaokoa na kuwa kona
Dk 1, Kamusoko anaachia shuti kali lakini kipa Aishi Manula anaokoa na kuwa kona, inachongwa na haina madhara
Dk 1 Mechi imeanza kila upande ukimvizia mwingine

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic