October 8, 2016



Kocha wa Simba, Joseph Omog, amepanga kuweka rekodi ya timu yake kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu bila ya kupoteza hata mechi moja.

Rekodi hiyo, iliwahi kuwekwa msimu wa 2009/10 na aliyekuwa Kocha wa Simba, Patrick Phiri, raia wa Zambia, ambaye aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa bila kufungwa.

Simba, yenye pointi 17, hadi hivi sasa ipo kileleni mwa ligi hiyo, ikiwa imecheza michezo saba ambapo imeshinda mitano na kutoka sare mara mbili dhidi ya JKT Ruvu na Yanga.

Omog alisema hilo linawezekana kutokana na maboresho, pia mbinu anazoendelea kuwapa wachezaji wake kila siku.
Omog, raia wa Cameroon, alisema kikubwa zaidi anawapongeza wachezaji wake kwa kushika mbinu na maelekezo anayowapa ndani ya uwanja na kuyafanyia kazi kwenye mechi zao walizocheza na kufanikiwa kutopoteza hata moja.

 “Tumemaliza mechi yetu na Yanga kwa sare, hivyo tunajiandaa na mazoezi makali ili timu ibaki kwenye ubora ninaouhitaji kuhakikisha tunaendelea kukaa kileleni.

“Kikubwa ninachokihitaji ni kuweka rekodi nzuri msimu huu nikiwa na Simba kwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu bila ya kupoteza mechi yoyote.


“Hayo ndiyo malengo yangu, na hilo linawezekana kutokana na wigo mpana wa kikosi changu kinachoundwa na wachezaji wengi nyota, hivi sasa ninawapa mbinu mbalimbali wachezaji wangu za jinsi ya kucheza kwenye viwanja vibovu kuhakikisha hatupotezi mechi yoyote,” alisema Omog.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic