October 6, 2016

KAMANDA MKUU WA KAMATI YA MASHINDANO YA SIMBA SC, MUSLEH AL RAWAHI.


Uongozi wa klabu ya Simba umeunda Kamati mpya ya Mashindano, ambayo itakuwa chini ya Mwenyekiti, Musleh Al Rawahi.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Haji Sunday Manara amesema katika Mkutano na Waandishi wa habari kuwa Kamati hiyo imeundwa ili kuongeza nguvu katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu.

Manara amesema pamoja na Musleh ambaye ni Mwenyekiti amewataja wajumbe wengine katika Kamati hiyo kuwa ni Makamu Mwenyekiti, Hassan Hassanoo na Wajumbe; Mohamed Nassor “kigoma”, Dk Cosmas Kapinga, Juma Abbas Pinto na Octavian Mushi.

Musleh ni kati ya wanachama wakongwe kabisa wa Simba na amekuwa anakumbukwa na wengi kutokana na ule uamuzi wake wa kumpa gari aliyekuwa kiungo wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ kutokana na juhudi na maarifa alizokuwa akionyesha wakati huo.

Kamati hiyo, imeelezwa itakuwa ikifanya kazi ya kuratibu masuala mbalimbali yanayohusiana na mashindano.

Musleh pia amewahi kuwa kwenye kamati ya usajili ya Simba na kamati nyingine mbalimbali.

Pia Hassanoo ambaye maarufu kama kama Mpiganaji, pia amewahi kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV