October 16, 2016


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amesema ukaribu wa viongozi wao pamoja na mashabiki umekuwa hamasa kwa wachezaji wa kikosi cha Simba kutaka kufunga mabao.

Kichuya amesema wao wanatamani zaidi kufunga na kushinda ili kuhakikisha mashabiki na viongozi wao wanakuwa na furaha.

“Kwa sisi washambuliaji au viungo, kazi yetu ni kufunga au kutengeneza mabao ili timu ifanye vizuri. Lengo letu ni kufanikiwa zaidi na kuisaidia timu.

“Wanachama na mashabiki, viongozi nao wako karibu nasi. Tunaona wanataka tushinde na sisi tunawaonyesha kwamba tuko tayari kuwa nao pamoja kupambana kwa ajili ya timu yetu,” anasema Kichuya.


Kichuya amefanikiwa kufikisha mabao saba katika mechi tisa alizoichezea Simba aliyojiunga nayo msimu huu akitokea Mtibwa Sugar.

2 COMMENTS:

  1. https://princeluanda.blogspot.co.ke/2016/10/top-five-watu-waliogeuka-matajiri-kwa.html?m=1

    ReplyDelete
  2. https://princeluanda.blogspot.is/2016/10/get-to-know-oldest-football.html?m=1

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV