October 16, 2016


Wachezaji wa Simba wameitwanga Kagera Sugar kwa mabao 2-0, baada ya hapo wakamuachia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kama zawadi.

Jana ilikuwa siku ya kuzaliwa ya Hans Poppe, hivyo wachezaji waliona kuwa ni siku nzuri ya kumpa zawadi kwa kushinda na wakafanya hivyo.

Hans Poppe mwenyewe anaonekana kufurahia kwelikweli zawadi hiyo ya ushindi wa mabao mawili kwa karai dhidi ya Kagera Sugar.

“Hakika ilikuwa siku nzuri sana kwangu, nimesherekea vizuri kabisa siku yangu ya kuzaliwa maana vijana wamenipa ushindi wa uhakika,” alisema Hans Poppe.

Poppe ndiye mwenyekiti wa usajili, maana yake ndiye anayehusika na usajili wa vijana hao walio Simba.

Kama haitoshi, amekuwa akijitolewa kutoa hamasa hata nje ya mkataba. Mfano kwa wachezaji wanaoonyesha uwezo na nidhamu kwa msimu mzima, wanaweza kuzawadiwa hadi magari.

Hans Poppe tayari amempa gari beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein Zimbwe. Na kama hiyo haitoshi, amenunua magari zaidi ya 15, tayari kuwazawadia wale watakaoonyesha uwezo na nidhamu hadi mwisho wa msimu.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV