ZEBEN (KULIA) NA MSAIDIZI WAKE |
Pamoja na kuwa Azam FC bado haina matokeo mazuri sana katika michezo yake mitano mfululizo msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kocha wa timu hiyo, Zeben Hernandez amesema bado wana nafasi ya kufanya vizuri.
Azam kwa sasa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kucheza mechi kumi na kupata pointi 13, ambapo imeshinda mechi tatu, imetoka sare nne na kufungwa mara tatu.
Zeben amesema kuwa: “Kinachotusumbua ni kukosa muunganiko mzuri wa timu kwani bado wachezaji hawajashika mbinu zangu, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri.”
Kocha huyo amekuwa akionekana ni mwenye juhudi za juu mazoezini kuwafundisha vijana wake kwa kuwaelekeza mambo mbalimbali.
Timu yake pia imekuwa ikionyesha soka safi lakini kazi kubwa imekuwa ni katika suala la umaliziaji hali inayoonyesha kuondoka kwa Farid Mussa na Kipre Tchetche ni sehemu inayochangia kiasi fulani kudorora kwa kikosi hicho katika ufungaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment