October 22, 2016Beki wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi amesema Simba inayoongoza ligi kuu kwa sasa imewashikia nafasi yao kwani muda wowote wataichukua.

Mwinyi aliyasema hayo hivi baada ya Yanga kuifunga Toto Africans mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Anasema ligi bado ni mbichi na tofauti ya pointi iliyopo siyo kubwa. Simba ipo kilele na pointi 26 wakati Yanga inazo 18.

“Ligi bado mbichi sana lolote linaweza kutokea, hivyo Simba wasijiamini kuwa ubingwa tayari wameshaupata ila wanatakiwa kujua kuwa nafasi waliyopo sasa wametushikia na siku yoyote tutaichukua.


“Tuna kikosi bora hivyo nawaomba mashabiki wa Yanga wasivunjike moyo ila wakae wakijua siku yoyote tutarudi katika nafasi yetu ambayo Simba wametushikia kwa muda,” alisema Mwinyi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV