October 15, 2016




MPIRA UMEKWISHAAAA

-Mavugo anaingia vizuri na kupiga shuti safi lakini Casillas anaonyesha umahiri mkubwa kabisa
-KADI Mwanjale analambwa kadi ya njano, ni kadi ya kipuuzi kwa kuwa aliupiga mpira nje wakati filimbi imeishapulizwa
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
KADI Dk 89, Mzamiru analambwa kadi ya njano kwa kufanya mashambo
Dk 89 sasa, wanachofanya Simba ni kumiliki mpira kwa kujiamini, ikiwa na maanda mabao mawili yanatosha na wanachofanya ni kuyalinda tu
Dk 86, Kichuya kwa mara nyingine anaachia mkwaju, lakini Casillas anaonyesha yuko njema, anadaka vizuri kabisa
SUB Dk 84, Simba wanafanya mabadiliko yao ya mwisho, Kazimoto anatoka nje na nafasi yake inakwenda kwa kinda Said Ndemla
Dk 81, mkongwe Kavila yuko chini, ameumia mguu wakati akirejea chini baada ya kuruka
GOOOOOOOO Dk 75, Shiza Kichuya anafunga bao lake la saba msimu huu huku akiandika la pili kwa Simba leo
Dk 74 PENAAAAAAAAAAAAT, Mohammed Ibrahim anawekwa chini na mwamuzi anasema ni tutaaa
Dk 72, Kagera wanafanya shambulizi zuri hapa lakini Juuko anaokoa, wanaingia tena kwa kasi, Bukungu anaokoa na kumpa mpira mrefu Mavugo, offside

Dk 69, MAvugo anaingia vizuri, nje ya boksi anapiga shuti kali kabisa lakini anashindwa kulenga lango
Dk 48, Mangona anapiga krosi safi lakini Juuko anaokoa na kuwa kona
Dk 68 sasa, mpira unaendelea kutawala zaidi katikati na viungo wanaonekana kutokuwa na pasi za hatari hasa katika umaliziaji
Dk 64, Mavugo anachomoka kwa kasi lakini anakuwa na papara na kupiga shuti nyanya na halijalenga lango
SUB 62 Kagera wanamalizia mabadiliko yao kwa kumtoa Mrwanda na nafasi yake inachukuliwa na mkongwe mwingine, Themi Felix 'Mnyama'

SUB Dk 60 Simba wanafanya mabadiliko ya pili wanamtoa Ajibu, wanamuinguza Mohammed Ibrahim 
Dk 59, Mkude anafanya kazi ya ziada kwa kuokoa mpira wa juu na kuwa kona. Inachongwa hatari kwenye lango la Simba, wanaokoa
SUB Dk 56, Simba wanafanya mabadiliko ya kwanza kwa kumtoa Blagnon na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo
Dk 54, mpira umesimama na Kazimoto anatibiwa hapa enka alilogongwa na Mangoma Suleiman wa Kagera

SUB Dk 52, anatoka Edward Christopher, anaingia mkongwe Paul Ngwai ambaye anasifika kwa mashuti ya mbali
Dk 51, Ally Nassor wa Kagera anageuka vizuri mbele ya mabeki wa Simba na kupiga shuti, lakini linakuwa nyanya kwa Angban
Dk 50 sasa, bado ushindani ni katikati ya uwanja na Kagera wanaendelea kuonyesha uhai hasa kwenye kiungo
Dk 46, mechi imeanza taratibuu kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza na Simba wanakuwa wa kwanza kufika langoni mwa Kagera

MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, pasi ndefu ya Mkude inamfikia Kichuya ambaye anapiga shuti kali lakini linatoka juu ya lango la Kagera
 GOOOOOOOOOOOOO Dk 44, Kona safi inachogwa na Muzamiru anafunga bao safi kabisa
Dk 43, krosi nzuri ya Kichuya, kichwa kinapigwa lakini Kagera wanaokoa na kuwa kona
Dk 41, Blagnon anaruka na kupiga kichwa lakini mpira unakwenda mikononi mwa Casillas
SUB Kagera wanamuingiza Ally Ramadhani na kumtoa  Mbaraka Yusuf 

Dk 37, Kazimoto anapiga shuti kali na linatoka sentimeta chache kutoka lango la Kagera. Hii ndio hatari kubwa kwenye lango la Kagera
Dk 37, Kagera wanachonga mpira wa adhabu lakini Muzamiru anafanya kazi ya ziada kuokoa
KADI Dk 36, Juuko Murshid analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mrwanda

Dk 26 hadi 31, Mpira hauna mashambulizi makali sana ya kutisha, lakini Kagera wanaonekana wepesi katikati ya uwanja wakiongozwa na Mangoma. Simba wanapenya katikati lakini mashambulizi yao si makali
Dk 23 sasa, bado mpira unachezwa katikati zaidi.Shuti lililolenga bao moja tu kutoka Simba kwenda Kagera na inaonekana umakini hasa kwenye kujihami, uko juu zaidi
Dk 18, Blagnon anaruka na kuunganisha mpira wa kona wa Zimbwe Jr, lakini Casillas anaonyesha umahiri na kudaka vizuri

Dk 14, Ajibu anaingia vizuri kabisa, lakini pasi yake kwa Bklagnon inakuwa fyongo
Dk 12, Kagera wanapoteza nafasi baada ya kugongeana zaidi ya pasi nane, lakini Mrwanda na Edward Christopher mwisho wanajichanganya na Bukungu anaokoa
Dk 5 hadi 10, Kagera wanaonekana kumiliki mpira zaidi. Hasa Mangoma na George Kavila, wanaonekana kutulia zaidi kuliko Muzamiru na Mkude kwa upande wa Simba

Dk 4, mabeki Kagera Sugar wanajichanganya, lakini kipa Sharrif anafanya kazi ya ziada na kuokoa. Inakuwa kona, inachongwa hata hivyo inaonekana haina manufaa kwa Simba
Dk 2, Simba wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Kagera lakini hakuna shambulizi kali kwa pande zote mbili hadi sasa.
Dk 1, mechi imeanza taratiibu na inaonekana kinachofanya kila timu imepania kuanza kupata bao la mapema.

3 COMMENTS:

  1. I high appreciate this post. It’s hard to find the good from the bad sometimes, but I think you’ve nailed it! would you mind updating your blog with more information https://dabong.net/xoilac-tv-%E2%80%93-kenh-truc-tiep-bong-da-online-cac-giai-dau-rat-hap-dan-t38337.html

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic