October 23, 2016

Mambo yanazidi kuwa magumu kwa Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola baada  kujikuta akishuhudia timu yake hiyo ikishindwa kupata ushindi katika mchezo wa tano mfululizo na mchezo wa tatu mfululizi katika Premier League.
 

Manchester City imelazimishwa sare ya bao 1-1 na wabishi Southampton kwenye mchezo wa Premier League ulipigwa leo kwenye Uwanja wa Etihad jijini  Manchester.


Southampton walianza kupata bao kupitia kwa Nathan Redmond katika dakika ya 27 kisha City wakasawzisha katika dakika ya 55 kupitia kwa Kelechi Iheanacho.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV