Dakika ya 90 + 4: Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inapata ushindi wa mabao 3-0, hapa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Dakika ya 90 + 2: Said Ndemla wa Simba anapiga shuti kali kutoka nje ya eneo la 18 la Toto lakini mpira unatoka nje.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anasimama, anaonyesha dakika 4 za nyongeza.
Dakika ya 87: Mchezo unaendelea.
Dakika ya 85: Mchezo umesimama kwa muda, beki wa Simba, Boukungu ameumia, anapatiwa matibabu.
Dakika ya 82: Mavugo anaingia na mpira kushoto mwa uwanja, anatoa pasi nzuri kwa Mnyate lakini beki wa Toto anwahi na kuokoa.
Dakika ya 75: Nahodha wa Toto, Salum Chuku anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo katikati ya uwanja.
Dakika ya 74: Mpira wa kona uliopigwa na Kichuya, unatua mguuni mwa Mzamiru, akiwa hajakabwa, anaipatia Simba bao la tatu kwa shuti kali ndani ya eneo la 18.
Mzamiruuuuuu GOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
Dakika ya 65: Simba wanafanya shambulizi kali, Kichuya na mpira lakini mabeki wa Toto wanaokoa.
Dakika ya 64: Simba wanapata kona, Kichuya anapiga lakini kipa wa Toto anaiokoa.
Dakika ya 62: Mchezo ulisimama kwa dakika mbili baada ya Mavugo kuumia wakati akiwania mpira na kipa wa Toto. Mchezo unaendelea.
Dakika ya 58: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mwinyi Kazimoto, anaingia Jamal Mnyate.
Dakika ya 55: Simba sasa wanaongeza kasi na wanamiliki mpira kuanzia katikati ya uwanja.
Dakika ya 52: Muda mfupi baada ya kuingia, Mavugo anaipatia Simba bao la pili, baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na Mohammed Ibrahim kutoka upande wa kulia.
GOOOOOOOOO!!!!! MAUGOOOOOOOOOOOOOOOO!
Dakika ya 49: Mchezo unaendelea, anaingia Mavugo anatoka Blagnon ambaye ameumia.
Dakika 48: Bado mchezo umesimama, Blagnon anaonekana amechanika kichwani.
Dakika ya 46: Blagnon ameumia kichwani na mchezo umesimama baada ya kugongana na beki wa Toto.
Kipindi cha pili kimeanza.
HALF TIME
Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza, Simba wanaongoa bao 1-0.
Dakika ya 45 + 3: Muda wowote mwamuzi atapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza.
Dakika ya 45 + 2: Simba wanapiga pasi nyingi na kuonekana kuelewana.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 44: Simba wanaongoza bao 1-0.
Dakika ya 43:Simba wanapata bao la kwanza, mfungaji ni Mzamiru, ambaye aliunganisha vizuri krosi iliyopigwa na Blagnon.
GOOOOOOOOOOOO!!!
Dakika ya 38: Kichuya anacheza vizuri baada ya kugongeana pasi na wenzake, anatoa pasi kwa Blagnon ambaye anabaki na kipa lakini anakuwa ameshaotea.
Dakika ya 37: Simba wanapata kona nyingine, lakini wanapiga na wanashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 30: Mchezo ni mkali na ushindani kwa kuwa kila timu inaonyesha kuwa na nguvu ya kutafuta bao. Ndiyo maana timu zot zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 27: Toto wanafanya shambulizi kali, Lusajo anashindwa kutumia nafasi baada ya kubabaika akiwa mbele ya lango la Simba.
Dakika ya 26: Simba wanapata kona nyinfine, Kichuya anapiga lakini inaokolewa.
Dakika ya 24: Simba wanafanya shambulizi kali, Blagnon anabaki yeye na kipa lakini anababaika na kuupaisha mpira baada ya kutokea kugongana kwa wachezaji wa Simba.
Dakika ya 19: Simba wanapata kona baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Mohamed Ibrahim, Kichuya anapiga kona lakini inaokolewa.
Dakika ya 16: Toto wanapata faulo nje kidogo ya eneo la 18 la Simba baada ya kucheza vizuri.
Dakika ya 13: Simba wanafanya shambulizi kali lakini kukosa umakini kwa Blagnon na Mzamiru kunawafanya wanapoteza nafasi hiyo waliyopata.
Dakika ya 11: Simba wanapata kona, Thsbalala anaenda kupiga lakini inaokolewa na mabeki wa Toto.
Dakika ya 10: Waziri Jr wa Toto anapata pasi anataka kuelekea lango la Simba lakini inakuwa no offside na mwamuzi anapuliza kipenga.
Dakika ya 7: Simba wanapata kona, beki Mohammed Hussein anaipiga lakini tayari kuna faulo imefanyika hivyo, mpira unapigwa kwenda lango la Simba.
Dakika ya 6: Mchezo bado haujawa na kasi lakini Simba ndiyo wanaomiliki mpira muda mwingi.
Dakika ya 3: Simba wanamiliki mpira muda mwingi, wamepiga pasi nzuri kuanzia katikati ya uwanja mpaka langoni mwa Toto lakini wakashindwa kumalizia kazi nzuri waliyoifanya.
Dakika ya 1: Mchezo umeanza hapa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mchezo unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.
Kikosi cha Simba kinachoanza leo hiki hapa:
1. Vicent Angban
2. Javier Bukungu
3. Mohamed Zimbwe
4. Method Mwanjale
5. Juuko Murshid
6. Jonas Mkude
7. Muzamiru Yassin
8. Mwinyi Kazimoto
9. Frederic Blagnon
10. Mohamed Ibrahim
11. Shiza Kichuya
SUB:
Denis (GK)
Hamadi Juma
Novart Kufunga
Jamal Mnyate
Said Ndemla
Ibrahim Ajibu
Laudit Mavugo
0 COMMENTS:
Post a Comment