October 23, 2016

MBAO FC

Prisons imegoma kupokonywa pointi zote tatu ikiwa nyumbani baada ya kusawazisha katika dakika ya 90 na kufanya matokeo dhidi ya Mbao FC kuwa 1-1.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, leo, hadi mapumziko hakukuwa na timu iliyokuwa imeziona nyavu za mwenzake.

Kipindi cha pili, mwanzoni bado kilionekana kuwa kigumu hadi Boniface Maganga alipoifungia Mbao bao katika dakika ya 84.

Baada ya hapo, Mbao walitumia muda mwingi wakipoteza muda na matumaini yalionekana kama wameishashinda.

Tayari zikiwa zimeonyeshwa dakika za nyongeza, Prisons walipata penalti na Lambert Sibianka akafanya kweli kwa kuipachika wavuni na kuwaacha askari magereza nao wakipata pointi dhidi ya kipenzi cha mafundi selemala kutoka Mwanza.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV