October 22, 2016


Leo jioni Yanga inacheza na Kagera Sugar mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kocha wa Yanga Hans van Der Pluijm amesema amezungumza na wachezaji wake kuhakikisha wanashinda.

Pluijm ambaye ni raia wa Uholanzi, timu yake ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, anaingia uwanjani kuikabili Kagera Sugar akiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Toto African wiki hii.

Kocha huyo amesema kuwa: “Licha ya uchovu, nimewaambia vijana wangu wapambane tushinde mechi hii ili tujiweke mahali pazuri katika kutetea ubingwa wetu.
“Vijana wamenielewa na kazi ilianza katika mechi dhidi ya Toto na sasa tunajipanga kuifunga Kagera ili kuweka matumaini ya ubingwa.”

Naye meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema majeruhi Amissi Tambwe na Andrew Vincent ‘Dante’ wapo vizuri na ni maamuzi ya kocha kuwatumia au vinginevyo.

Naye Kocha wa Kagera, Mecky Maxime alisema atapambana kuhakikisha Yanga haiondoki na pointi tatu kwani nao wanataka kupaa kwenda nafasi ya pili.

Kagera ipo nafasi ya nne nyuma ya Yanga lakini zote zina pointi 18 lakini zinatofautiana mabao tu. Hata hivyo, Kagera imecheza mechi 11 wakati Yanga imeshuka uwanjani mara tisa tu.
“Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho (leo), najua Yanga ni timu nzuri, lakini binafsi naiona timu ya kawaida na inafungika. Tunataka tushinde tukae nafasi ya pili,” alisema Maxime.


MSIMAMO LIGI KUU:

Nafasi    Timu       Pointi
1              Simba     26
2              Stand      20
3              Yanga     18

4              Kagera    18

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic