October 22, 2016


Pamoja na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuwataka wanachama wa Yanga kuwa watulivu mara baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, lakini amehoji waliokwenda mahakamani kama wameshindwa kulipa ada ya Sh 1,000 kwa mwezi, wanaweza vipi kulipa ada ya wakili!

Wanachama wa Yanga waliopeleka zuio hilo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu ni Frank Chacha na Juma Magoma.

“Jiulize wanashindwa kulipa shilingi elfu moja kama ada, lakini wanapata fedha ya wakili kwa ajili ya kuweka zuio la mkutano,” alisema.

"Haiwezi kuwa hivihivi, lakini kutakuwa na jambo nyuma ya pazia."

Hata hivyo, Manji alisema waliopeleka zuio hilo la mkutano si wanachama kwa kuwa Frank Chacha hajalipia ada yake kwa zaidi ya miezi sita na mwingine Juma Magoma pia si mwanachama wa Yanga kwa kitambo sasa.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV