October 22, 2016


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewataka wanachama wa Yanga kuwa watulivu mara baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, kuzuia mkutano wa dharura uliopangwa kufanyika kesho kwenye makao makuu ya klabu hiyo.

Manji amezungumza na waandishi wa habari leo na kusema walipata zuio hilo la mahakama zaidi ya saa 12:30 jioni, jana.

“Tukalazimika kufanya uhakiki kama ni kweli, mwisho tukagundua ilikuwa ni kweli. Tuwaombe radhi hata kama waliozuia mkutano wetu si wanachama. Tunaamini itafikia siku, tutakutana kwa kuwa mkutano ni haki yetu ya msingi.

“Utulivu ni jambo jema, lazima tuonyeshe ukweli kuwa sisi ni watulivu, waelewa lakini tutekeleze uamuzi huo wa mahakama huku tukisubiri siku yetu itafikia na kila kitu kitafanyika kwa utaratibu.

“Waliokuwa mikoani, wabaki na siku mkutano ukiwepo watafika kwenye mkutano. Yanga ni klabu inayohusika na historia ya nchi hii, hivyo lazima tuwe msitari wa mbele kuimarisha amani,” alisema Manji.

Hata hivyo, Manji alisema waliopeleka zuio hilo la mkutano si wanachama kwa kuwa Frank Chacha hajalipia ada yake kwa zaidi ya miezi sita na mwingine Juma Magoma pia si mwanachama wa Yanga kwa kitambo sasa.

Aidha, alisisitiza hata hao waliokwenda mahakamani kama wangekuwa wanachama hai, basi wangekuwa wameishajifuta rasmi baada ya kwenda mahakamani kwa kuwa katiba ya Yanga inakataza kwenda mahakamani kama ilivyo kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic