October 19, 2016


Nahodha na kiungo wa Simba, Jonas Mkude, ameweka wazi kwamba jambo ambalo linawatesa kwa sasa ni kuhakikisha wanaendelea na rekodi yao ya kuifunga kila timu wanayokutana nayo ili mwisho watimize ahadi ya kuwavua ubingwa mahasimu zao Yanga.

Mkude mpaka sasa ameifanikisha Simba kuongoza ligi ikiwa na pointi 23 baada ya mechi zake tisa wakiwa mbele ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi kwa pointi nane. Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 15.  

Kiungo huyo amesema sasa wana kazi kubwa ya kuendeleza ushindi kwa kila timu ambayo watakutana nayo kuanzia Mbao FC, watakaocheza nao kesho Alhamisi kwa ajili ya kuvuna pointi nyingi ambazo zitawasaidia kwenye kampeni yao ya kutwaa ubingwa kwa msimu huu.

“Kila mchezo kwetu ni fainali na tunacheza kwa kujitoa kuhakikisha kwamba tunashinda na kupata pointi tatu iwe isiwe na hilo tuna uhakika kwamba kila kitu kitatimia kwa sababu tunahitaji ubingwa kwa msimu huu baada ya kupita misimu mitatu sasa tukitoka kapa.


“Yaani yeyote yule ambaye anakuja mbele yetu haitajalisha ana uwezo wa aina gani sisi tutapigana naye kuhakikisha tunamfunga na hata hawa Mbao FC ambao tunacheza nao mechi inayokuja, wajiandae kwa kichapo kutokana na kutaka kuendeleza rekodi yetu ya kutofungwa na kupoteza pointi, jambo ambalo linaweza kutupotezea malengo yetu ya kuuchukua ubingwa,” alisema Mkude.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV