October 18, 2016


Simba ambayo inakwenda “mwendo kasi” kwenye Ligi kuu Bara, imefanya mazoezi yake ikiendelea kujiwinda kabla ya kuwavaa Mbao FC.

Kazi ya kupambana na Mbao FC ambao wameonekana ni wabishi kwelikweli, itakuwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Vetarani jijini Dar es Salaam na wachezaji walionekana ni wenye furaha na wako tayari kwa ajili ya mechi ya kesho.

Simba ndiyo inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 9 za ligi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV