October 19, 2016



Yanga ina kazi nyingine leo, inacheza na Toto African katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, lakini timu hiyo mwenyeji imesema haitakubali kufungwa lakini lolote litakalotokea ni sehemu ya mchezo na si vinginevyo.

Kocha wa Toto, Khalfan Ngassa ambaye ni baba mzazi wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa, ameliambia Championi Jumatano kuwa, kikosi chake kipo fiti kucheza na Yanga na lengo lao ni kupata ushindi.

"Tumefanya mazoezi makali ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo wetu wa Jumatano (leo) dhidi ya Yanga, kikosi kipo sawa labda tushindwe wenyewe tu.

“Naomba nieleweke hapa kwamba kitakachotokea katika mchezo huu ni matokeo ya mchezo kwani hatujajiandaa kufungwa na Yanga ila siwezi kuwaahidi Wanamwanza chochote kuhusiana na mechi hii,” alisema Ngassa.

Wakati Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 15 katika michezo nane, Toto yenyewe ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi 10. Kabla ya mchezo huu, Yanga ilitoka suluhu na Azam wakati Toto ilifungwa mabao 2-1 na Majimaji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic