Stand United wametamba kwamba wana uwezo wa kufanya vizuri bila ya kocha wao, Patrick Liewig raia wa Ufaransa.
Liewig amesusa kuitumikia Stand United iliyo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa madai kwamba hajalipwa fedha zake.
Msemaji wa Stand United, Deokaji Makomba amesema wanaweza kuendelea na kocha wao, Athumani Bilal ‘Bilo’.
“Tuko na Bilo, anaendelea na kazi vizuri na hatuna hofu hata kidogo,” alisema.
“Tunaamini Bilo amekuwa siku nyingi na timu hii anaijua vizuri sana na ataendelea kufanya vizuri.”
Baada ya wadhamini wa Stand, Acacia kusitisha mkataba wao na klabu hiyo, suala la ugumu wa malipo likaibuka na kuzua ugumu.
Kutokana na kucheleweshewa malipo, Liewig akaamua kuondoka zake na haijulikani alipo.
0 COMMENTS:
Post a Comment