KESSY |
Bosi wa Sputanza, Mussa Kisoki amesema amekuwa akishangazwa na Yanga, kwa nini hawamtumii beki wao, Hassan Kessy.
Kisoki amesema anavyojua Kessy ameruhusiwa kuendelea kuichezea Yanga wakati kesi yao dhidi ya Simba ikiendelea.
“Mimi najua Kessy hana tatizo na aliruhusiwa kucheza. Sasa Yanga wenyewe wanajua kwa nini tena wanamuweka nje.
“Lakini kama unavyokumbuka, kamati imewaruhusu wamtumie. Hivyo sioni kama kuna tatizo tena,” alisema Kisoki.
Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba, Yanga imeamua kuacha kumtumia Kessy ikiingiwa na hofu kwamba inaweza kushindwa kesi yake dhidi ya Simba ambayo inalalamika beki huyo kuvunja mkataba.
Simba inailalamikia Yanga kumsajili Kessy huku ikijua ana mkataba wa Simba.
STITANZA kweli hamjielewi. Sasa mnadhihirisha mapenzi yenu kwa yanga bila kuwaza kwa kina nini kitatokea hapo baadaye.
ReplyDelete