October 17, 2016Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza kuwa tayari limefanikiwa kuzikomboa nyasi bandia kwa ajili ya Uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza.

Nyasi hizo bandida zimekombolewa bandarini ambapo zilikwama kwa zaidi ya mwaka na nusu.


Msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amethibitisha hilo alipozungumza na SALEHJEMBE.

“Tunapenda kuwahakikishia Wanamwanza kwamba tamari tunazo nyasi bandia mkononi, hivyo sasa ni suala la hatua tu ili zianze kutumika kwenye uwanja wa Nyamgana.


“Tunasubiri mtaalamu kutoka Fifa ambaye atafanya kazi za uwekaji wa nyasi hizo,” alisema Lucas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV