Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm alipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wawili wa Azam FC, Kipre Bolou na Serge Wawa raia wa Ivory Coast kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Jambo hilo limezua gumzo hiyo jana, pia leo kwamba mara baada ya mechi kati ya Azam FC ikiikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru, vipi ilikuwaje hadi Pluijm akaamua kuzungumza nao muda takribani dakika 10.
Tena inaonekana wakiwa kwenye kona na inaelezwa kwamba mkataba wa wachezaji hao unaenda ukiingoni.
Inawezekana ni salamu tu, lakini watatu kati yao kila mmoja amelifanya jambo hilo ni la kawaida na hakuna haja ya kulifafanua.
Hata hivyo, wakati Pluijm akizungumza nao, mfanyakazi mmoja wa Azam TV, hakupanduka karibu yao huku akisikiliza kwa umakini kwelikweli.
Wawa ambaye ni beki wa kati na kiungo Bolou ni kati ya wachezaji wa Azam FC wanaosumbuliwa na majeruhi.
0 COMMENTS:
Post a Comment