TOTO |
Kikosi cha Toto African, kimetamba kwamba kitawatoa shoo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga.
Yanga ipo mjini Mwanza kuwavaa Toto katika mechi ya Ligi Kuu Bara, mechi itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Msemaji wa Toto, Cathbert Japhet amesema wana imani kubwa kwamba wako vizuri.
“Tunaamini Yanga hawataondoka na pointi kesho. Timu yetu ipo vizuri na tumejiandaa kweli.
“Maandalizi yetu yako vizuri na tunaomba kesho msubiri kuona tutakachofanya,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment