October 15, 2016



Kuna uwezekano mkubwa beki wa Yanga, Hassan Kessy akashuka kiwango chake na kupotea endapo sakata lake halitapatiwa ufumbuzi mapema.

Kessy aliingia mgogoro na Simba kufuatia kuanza kuitumikia Yanga huku akiwa bado hajamaliza mkataba wake na klabu yake hiyo ya zamani. Kutokana na hali hiyo, Simba wakashitaki suala hilo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Uamuzi wa awali wa TFF unamtaka Kessy kuilipa Simba ambapo ulizitaka klabu hizo kukaa na kumalizana juu ya suala hilo lakini klabu hizo mbili hazijakutana kujadiliana.
Badala yake kila timu imewasilisha barua ambazo hazijafanyiwa kazi hadi sasa.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, amesema hadi sasa suala la Kessy halijajulikana litasikilizwa lini kwani Kamati ya Katiba, Maadili na Hadhi za Wachezaji haijulikani itaketi lini.
“Tumepokea barua kutoka Simba na Yanga kuhusu suala la Kessy baada ya kushindwa kulimaliza wao wenyewe, lakini hadi sasa barua hizo zipo ofisini na hazijafunguliwa hadi pale kamati hiyo itakapokutana.

“Haijulikana kamati hiyo itakaa lini ili kujadili suala hilo kwa kuwa bado hatujapanga, kwani asilimia kubwa ya wanakamati si waajiriwa wa TFF hivyo ni mpaka wapate nafasi,” alisema Lucas.

Jana asubuhi Kessy alionekana akifanya mazoezi na Yanga ambapo alisema anaumizwa na jinsi suala lake linavyokwenda huku akiwa haelewi kwa nini anawekwa benchi.


Taarifa nyingine zinaeleza kuwa Yanga haitaki kumtumia Kessy ikihofia matatizo siku za mbele kwani suala lake bado halijapatiwa ufumbuzi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic