October 15, 2016



Hamadi Juma alikuwa beki wa kulia tegemeo kwenye kikosi cha Simba, sasa katika nafasi yake kaja Besala Bokungu ambaye anachukua namba ‘deile’, sasa Hamad kaamua kupiga tizi mara mbili kwa siku.

Hamad ameweka programu ya kufanya mazoezi mara mbili kwa siku kwa kipindi ambacho wanakuwa mapumziko lengo lake likiwa ni kuweka sawa kiwango chake ili arejee ‘first eleven’.

Beki huyo amecheza mechi moja tu dhidi ya Ndanda FC ambayo Simba ilishinda mabao 3-1, lakini baadaye akapata jeraha alipoanguka chooni na kupasuka kichwani na tangu hapo hajacheza tena.

Baada ya Hamad kuumia, kwanza alitumika Malika Ndeule katika nafasi ya beki ya kulia halafu akaja Bokungu raia wa DR Congo ambaye anatesa hadi leo.

Hamad aliyesajiliwa msimu huu kutoka Coastal Union, amesema ameamua kufanya mazoezi mara mbili siku ambazo wanapumzika na anajiongezea mara moja wanapofanya mara moja.

“Bokungu alipata namba baada ya mimi kuumia, napigana kuhakikisha ninarejesha namba yangu. Nimeamua kupiga tizi kivyangu, mfano kama siku tukiwa na programu moja ya mazoezi huwa naenda gym.

“Nasaka stamina mchangani mfano pale Coco (ufukweni) huwa naenda kwa siku ambazo hatupo kambini,” alisema Hamad.

“Hata hivyo, kuna vitu vingi huwa najifunza kutoka kwa Bokungu kwani yeye ni mkongwe na amekuwa kwenye soka muda mrefu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic