November 18, 2016


Uongozi wa Azam FC umebakiza usajili wa wachezaji watatu tu katika dirisha dogo.

Wachezaji wawili watakuwa ni hapa nyumbani na mmoja kutoka nje ya nchi lakini imeapa, kamwe haitasajili mchezaji kutoka Yanga au Simba.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba Byemba amesema wamekubaliana, Simba na Yanga, waendelee na mambo yao.

"Kweli hili tumekubaliana wenzetu waendelee na yao na sisi tufanye yetu. Tunaendelea na kufanya ytaratibu kupitia katika njia yetu.

"Tumebakiza nafasi moja ya mchezaji kutoka nje, pia tunataka wachezaji wawili kutoka hapa," alisema Kawemba.

Tayari Azam FC imeanza masuala ya usajili kwa kusajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania. Imesajili washambuliaji wawili kutoka Ghana.

Kikosi cha Azam FC chini ya Mhispania Zeben Hernandez hakikuwa na mwanzo mzuri mwanzoni mwa Ligi Kuu Bara lakini kikaanza kubadili mwendo mwishoni mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV