November 4, 2016




Kocha wa Taifa Stars ametangaza kikosi chake kitakachoivaa Zimbabwe katika mechi ya kirafiki huku Simon Msuva akiwa mchezaji pekee kutoka Yanga kwa upande wa viungo wa ushambulizi.

Mkwasa amewachota viungo wapya ambao wengi wao walionekana hawana nafasi awali. Kwa upande wa Yanga, mchezaji mwingine aliyeitwa ni Haji Mwinyi ambaye amekuwa na kiwango kizuri hivi karibuni.

Mkwasa ameita jumla ya nyota 24 ambao watasafiri kuifuata Zimbabwe Novemba 12, mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo ulio kwenye kalenda ya Fifa.

Aidha, Mkwasa ameingiza sura mpya kama, fowadi Omary Mponda wa Ndanda, kipa Said Kipao na beki Aidan Michael (JKT) na beki James Josephat wa Prisons na kuwatema masta kama Deus Kaseke, Kelvin Yondani, Hassan Kessy (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Aboubakar, Aggrey Morris (Azam).

Akitangaza kikosi hicho, Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema: “Kikosi kitaingia kambini siku moja baada ya raundi ya kwanza kumalizika, yaani Novemba 7 mpaka Novemba 11 kabla ya kusafiri kesho yake kuifuata Zimbabwe.”


MAKIPA: 
Aishi Manula (Azam), deugratius Munishi (Yanga) na Kipao (JKT Ruvu).

MABEKI:
Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam), Michael (JKT), Vicent Andrew, Haji Mwinyi (Yanga) na Josephat (Prisons).

VIUNGO:
Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’, Jamal Mnyate na Yassin Mzamiru (wote Simba) Himid Mao (Azam) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).

WASHAMBULIAJI:
John Bocco (Azam), Ibrahim Ajibu (Simba), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Elias Maguri (Dhofar, Oman), Thomas Ulimwengu (huru) na Omary Mponda wa Ndanda.

Lucas alisema kutokana na mbanano wa michezo, mechi za viporo Simba vs Prisons, Yanga vs Ruvu Shooting na Mwadui vs Azam, zote zimepangwa kupigwa Novemba 10.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic