Mwadui FC sasa ipo chini ya Khalid Mohammed ambaye ametamba timu yake kutisha katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Mohammed amechukua nafasi ya Jamhuri Kihwelo 'Julio' ambaye 'alikimbizwa' na waamuzi wasiotenda haki.
Mohammed amesema wakati huu ambapo ligi imesimama, amewapa mapumziko mafupi vijana wake kisha watarejea kwa mazoezi makali kambini kwao na ana imani watafanya vizuri mzunguko wa pili.
Mwadui ipo katika nafasi ya 15 katika ligi ambayo si nzuri ikiwa na pointi 13 katika mechi 15 ilizocheza ambapo imeshinda tatu, imetoka sare nne na kufungwa mara nane.
Mohammed amesema kuwa: “Unajua siyo kila msimu timu inakuwa na matokeo mazuri, hii hali inaweza kuitokea timu yoyote ile, sasa tunaenda kujipanga.
“Katika kikosi kuna upungufu mdogo nimeubaini, hasa kwenye kiungo na ulinzi, tutakitumia kipindi kijacho cha usajili wa dirisha dogo kuimarisha kikosi, naamini mzunguko wa pili tutakuwa vizuri.”
0 COMMENTS:
Post a Comment