December 4, 2016



Mshambuliaji nyota wa Man City, Kun Aguero atakosa mechi nne za Ligi Kuu England baada ya kufanya rafu ya kijinga dhidi ya beki David Luiz wa Chelsea.

Chelsea iliitwanga Man City kwa mabao 3-1 na Aguero akamrukia Luiz katika dakika ya 90. Pamoja na kadi nyekundu, FA imeamua akose mechi hizo nne.


Wakati Aguero anakosa mechi nne, kiungo Fernandinho naye atakosa mechi tatu akitumikia adhabu ya kumkaba kooni na kumsukuma hadi chini kiungo Cesc Fabregas.

Luiz amekataa katakata kulizungumzia suala kwamba, huenda amekuwa na ugomvi na Aguero ambaye katika mechi hiyo, yeye alianza kumngonga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic