Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, gumzo ni wachezaji wawili, Simon Msuva wa Yanga na Jonas Mkude wa Simba.
Wawili hao wanaonekana wakiwa katika gari moja, wengi mtandaoni wanaichukulia kama sehemu kuwa huenda Mkude ndiyo njiani kujiunga na Yanga kwa kuwa suala lake la usajili na Simba linaonekana kuwa na shida.
Kiuhalisia, Mkude na Msuva ni marafiki wa karibu kwa kuwa wote wako katika umri mmoja ‘aga mate’ na wamecheza pamoja sehemu mbalimbali kwa maana ya upinzani lakini wakiwa pamoja mfano timu za vijana na taifa.
Ingawa watu hawajaeleza au kujua kwamba picha hiyo ni ya hivi karibuni au ya kitambo.
Wanaojadili mitandaoni, wengi wanaamini Msuva anaweza kumshawishi kutua Yanga. Wako wanaomkaribisha na wengine wakionyesha hawana shida naye Yanga.
Kwa mashabiki wengi wa Simba, wengi wanapuuza kwa kusema “aende zake”, wako wanaonya kwamba awaangalie akina Ramadhani Singano na wengine na wengine wanamshauri kuwa makini wakiamini Yanga huua vipaji vya wachezaji wengi wanaotokea Simba. MJADALA UNAENDELEA.
Najaribu kuangalia baadhi ya wachezaji waliotoka Simba kwenda Yanga kama vile Lunyamila, Athumani Chuji na Amisi Tambwe walivyotoka Simba sioni namna vipaji vyao vilikufa au kushuka. Vipaji au viwango vya wachezaji wa Kitanzania vinatokana na kasumba ya kujiona hawana kiu ya mafanikio zaidi ya Simba na Yanga na mashabiki wa kitanzania hatuwaoneshi kitu tofauti na kuwajuza juhudi zao ni muhimu zaidi...
ReplyDeleteNi maisha yake, ana uamuzi wa kucheza popote kwani ameshapoteza matumaini ya kucheza Proffessional Football na toka aanze game yupo Simba, tunategemea aende wapi kumalizia mpira wake zaidi ya Yanga!!! Nenda kaoige dili uishie zako kama akina Ngassa na wengine kibao!! SIMBA NGUVU MOJA, KATA MTI PANDA MTI!
ReplyDelete