December 4, 2016

Wanachama na mashabiki wa Yanga wakiwemo wanamichezo mbalimbali wamemuombea na kumsalia Yusuf Mzimba (84) na baadaye mwili wake umesafirishwa kwenda Msoga.

Lakini utani umeibuka msibani baada ya watani wa Yanga, mashabiki na wanachama kuanza kuwatania wenzao kutokana na kuusafirisha mwili wa mwanachama wao huyo mkongwe kwa roli aina ya Canter.

Mashabiki wa Simba walikuwa wakiwatania wenzao wa Yanga, kwamba wanataka kufanya mabadiliko wakati wanashindwa kutoa hata fedha ya Toyota Coaster kuusafirisha mwili wa gwiji huyo wa Yanga.

Mzimba anakumbukwa kwa umahiri wake wa kuwapigania Wanayanga wa muda mrefu wakati wa kipindi cha mvutano mkubwa kati ya Yanga Kampuni na Yanga Asili aliyokuwa akioongoza.











0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic