CHACHA |
Waliokuwa maafisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Juma Matandika na Martin Chacha, leo Jumatatu wanatarajiwa kupanda tena kizimbani kwa mara ya tatu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar wakikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa.
Matandika ambaye alikuwa msaidizi wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, huku Chacha akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano ya TFF, wanakabiliwa na kesi hiyo inayodaiwa kutendeka Februari 4, mwaka huu.
Inadaiwa kuwa, siku hiyo, wawili hao waliomba rushwa ya Sh milioni 25 kwa viongozi wa timu ya Geita Gold Sports, Salum Kulunge na Constantine Molandi ili kuisaidia kupanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita.
Leo Jumatatu, upande wa mashitaka ambao ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), shahidi Sosthenes Kibwengo ambaye ni mchunguzi mkuu wa Takukuru baada ya kuwasilisha ushahidi wake wiki iliyopita, atahojiwa na upande wa washtakiwa kuthibitisha ushahidi wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment