December 5, 2016



Kamati ya Usajili ya Simba chini ya mwenyekiti wake Zakaria Hans Poppe, imesema kuwa kwenye usajili wao wa dirisha dogo la usajili, ni lazima wamsajili beki mwingine mwenye uwezo kama Mganda, Juuko Murshid.

Dirisha dogo la usajili tayari limefunguliwa tangu Novemba 15 na litafungwa Desemba 15, mwaka huu kwa timu zote shiriki za Ligi Kuu Bara.

Nafasi hiyo ya beki wa kati inayochezwa na Juuko, huwa inachezwa pia na Emmanuel Semwanza na Novalty Lufunga.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Hans Poppe alisema watamsajili beki wa kati mwingine, kwa kuwa watamkosa Juuko kwa miezi miwili kutokana na kutakiwa kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) inayotarajiwa kufanyika Januari, mwakani.

Hans Poppe alisema, beki huyo wanayemhitaji ni yule atakayeweza kupambana na washambuliaji wasumbufu.
“Tunatarajia kumkosa Juuko kwa kipindi cha miezi miwili atakachokuwepo na majukumu ya timu yake ya taifa ya Uganda itakayokuwa inashiriki michuano ya Afcon.

“Hivyo, anatarajia kuzikosa baadhi ya mechi za mwanzoni za mzunguko wa pili wa ligi kuu, hivyo ni lazima tumtafute beki mwingine mwenye sifa kama zake za kupambana na washambuliaji wasumbufu.

“Kama kamati husika, hivi sasa tupo kwenye michakato ya kumsajili beki huyo tunayemhitaji atakayecheza pamoja na beki wetu, Mwanjale (Method) katika kipindi ambacho Juuko hayupo,” alisema Hans Poppe.

SOURCE: CHAMPIONI



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic