December 5, 2016



Simba imekubaliana kila kitu na kipa wa zamani wa Medeama ya Ghana na leo hii wanamalizana.

Kipa Daniel Agyei anatarajia kusaini mkataba wa kuichezea Simba leo.

"Kila kitu safi na leo ndiyo tunamalizana na Agyei. Tulifanya mazungumzo jana na juzi na yeye amekubali," kilieleza chanzo.

Taarifa zinaeleza, kipa huyo alisema hawezi kufanya mazoezi na Simba hadi hapo atakaposaini mkataba.

"Alisema hajaja kwa ajili ya majaribio, hivyo hadi asaini mkataba leo, kesho ataanza kazi."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic