January 27, 2017

Muda mfupi baada ya serikali kupitia Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kutangaza kuufungulia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya matumizi ya michezo na shughuli nyingine za kijamii, Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetoa tamko.

TFF imetangaza kuwa kutokana na ruhusha hiyo, sasa michezo ya wikiendi hii inayozihusisha Simba na Yanga ni rasmi itafanyika kwenye uwanja huo ambao ni mkubwa kuliko vianwaj vyote vya michezo nchini.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema:

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas

Mashabiki wa Yanga na  Simba.


“Nachukua nafasi hii kumshuru rais wetu Magufuli na serikali kwa jumla kwa kuweza kuamua kuufungua Uwanja wa Taifa uanze kutumika na timu za Simba na Yanga ambazo zilifungiwa kuutumia.

“Nimpongeze Waziri Nape Nnauye kwa juhudi zake za kuweza kumshawishi rais kukubali kuruhusu kwa timu hizo kuendelea kuutumia.

“Hivyo sasa mchezo wa kesho kati ya Azam na Simba utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, nitoe wito kwa mashabiki na wadau wa soka kwamba uwanja umefungwa kamera za kisasa ambazo zitaweza kubaini matukio yote yatakayokuwa yakijitokeza na ikukumbwe vyombo vya usalama vina mkono mrefu, sasa ni bora tukashirikiana wote kwa pamoja kuutunza.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic